Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC HAITAKI KULALA,YAMPA MKATABA WA MIAKA 2 MCHEZAJI HUYU, "USIKU"

  Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.12,2015 SAA 12:48 JIONI

Taarifa kutoka katika Tovuti Rasmi ya Simba Sports Club (SSC),zinasema kuwa klabu hiyo imemsajili rasmi kiungo wa
kimataifa Justine Majabvi akitokea katika timu ya Vicem Hai Phong F.C nchini Vietnam pia alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe,kwa ajili ya kuendeleza mkakati wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.


Majabvi amewahi kuwa mwanasoka bora wa Zimbabwe mwaka 2005, 2007 na mwaka 2008.
Kati ya mwaka 2008 – 2009 Majabvi alichezea timu ya Lask Linz FC ya Austria pia amewahi kucheza nchini Ujerumani kabla ya kuchezea Vicem Hai Phong F.C nchini Vietnam.
Justine Majabvi ambaye mashabiki na wapenzi wa Simba walipata nafasi ya kumwona akichezea Simba siku ya Simba Day,na jana usiku tarehe 12 – 8 – 2015 amesaini rasmi mkataba wa kuichezea Simba kwa muda wa miaka miwili.
Majabvi alizaliwa tarehe 26 – 3 – 1984 Harare Zimbabwe aliwahi kuicheza Klabu ya Lancashire Steel F.C ya nchini Zimbabwe mwaka 2002 – 2005, Dynamos Football Club (Dynamos Harare) ya nchini Zimbabwe mwaka 2006 – 2008 na Khatoco Khánh Hoà ya nchini Vietnam mwaka 2012.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments