KUSHOTO: Hassan Kessy akiwa na Juma Abdul (picha na barakampenja.com) |
Uongozi wa klabu ya Young Africans, umeendelea kuwatumia ujumbe viongozi wa klabu ya Simba, ambao wanadaiwa kugoma
kutoa barua ya kumruhusu beki wa pembeni Hassan Kessy, ili aanze kuwatumikia mabingwa hao wa soka Tanzania bara kwenye michuano ya kombe la shirikisho.
Young Africans walishindwa kumtumia beki huyo waliyemsajili siku chache kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2015-16 mwezi uliopita kwa kigezo cha mkataba kati ya Hassan Kessy na Simba kufikia kikomo.
Afisa habari wa Young Africans Jerry Muro, amesema jambo ambalo linaendelea kufanywa na viongozi wa Simba la kushindwa kuwapa ushirikiano wa kuandika barua ambayo itamuidhinisha Kessy kuanza kuwatumikia wanajangwani, sio la kiungwa na halipo katika misingi ya kizalendo.
Wakati huo huo Jerry Murro amezungumzia mustakabali wa beki wao wa kulia Juma Abdul ambaye alishindwa kujumuika na wachezaji wenzake wa Young Africans katika maandalizi pamoja na mchezo dhidi ya Mo Bejaia kutokana na mejeraha yaliyokua yanamkabili.
SIKILIZA HAPA
W
0 Comments