Wachezaji wa nne wa Timu ya Taifa ya Riadha wameagwa na kukabidhiwa Bendera hii leo kwa ajili ya kwenda Beijing
nchini China kushiriki mashindano ya dunia ya Riadha yatakayofanyika tarehe 22 mwezi huu.
nchini China kushiriki mashindano ya dunia ya Riadha yatakayofanyika tarehe 22 mwezi huu.
![]() |
| wachezaji wakifanya maombi kwa ajili ya mashindano. |
![]() |
| ,Mkurugenzi wa Msaidizi wa maendeleo ya Michezo,Bi Juliana Yasoda akikabizi bendera ya taifa kwa wachezaji. |
Akikabidhi Bendera hiyo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa Msaidizi wa maendeleo ya Michezo,Bi Juliana Yasoda amewataka wanariadha hao kutambua kuwa wao ni mabalozi wa watanzania na ndio maana wamekabiziwa bendera kwa ajili ya kwenda kuwawakirisha vizuri watanzania.
Bi Juliana Yasoda pia amesema mara baada ya kurudi kwa wanariadha hao,kambi haitavunjwa bali watarudi kambini kwa ajili ya kujiandaaa na mashindano mbalimbali.
![]() |
| wachezaji wakifanya maombi kwa ajili ya mashindano hayo. |
![]() |
| mkutano ukiendelea. |
Naye Fransis John ambaye ni kocha wa wachezaji hao wa timu ya Taifa inayokwenda Beijing nchini China katika mashindano ya dunia ya Riadha amesema wachezaji wake amewapa maandalizi ya kutosha na kuahii kurejea na medali.
Nao wanariadha wanaokwenda Beijing nchini China katika mashindano ya dunia ya Riadha wameahidi kufanya vizuri katika mashindano hayo




0 Comments