Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:SIMBA NA YANGA WALIVYOKIPIGA TAIFA,USHIRIKINA HADHARANI

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.18,2014 SAA 06:30  USIKU


Mchezo namba 27 wa Ligi Kuu ya Vodacom uliowakutanisha watani wa jadi Young Africana kutoka eneo la Jangwani na
Simba SC kutoka eneo la msimbazi jijini Dar es salaam umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana (0-0), mtanange uliofanyika jioni ya leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 









Young Africans ilingia uwanjani chini ya kocha wake Marcio Maximo kusaka pointi tatu hali kadhalika Phiri wa Simba akisaka alama tatu pia hali iliyopelekea mchezo huo kuwa mgumu kutikisika kwa nyavu za pande zote mbili.  





Kocha mbrazil alimtumia mshambuliaji Jaja akisaidiwa na Coutinho, Ngasa, Niyonzima na viungo Mbuyu Twite na Hassan Dilunga huku Phiri akimtumia Maguri kama mshambuliaji kiongozi akisaidiwa na Kiemba, Ndemla, Chanongo na Okwi.

Simba ilifanya mashmabulizi langoni wa Young Africans kupitia kwa washambuliaji wake Okwi, Maguri na Chanongo lakini jitihada zao hazikuzaa matunda na kukuta mipira yao ikiishia mikononi wa mlinda wa Deo Munish "Dida" na mingine kupaa juu ya lango au kuokolewa na walinzi.  Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Simba SC.


Katika mchezo huo poa kumejitokeza kwa vitendo vya ushirikina ambavyo vimekuwa vikipigiwa kelele kila siku,ambapo kumepatikana kwa vipande vya maganda ya mayai vilivyokuwa vimeandikwa kwa elufi za kiarabu.

ANGALIA PICHA ZA MCHEZO ULIVYOKUWA 









































Lineups 
Simba: Manyika Pater, William Lucian, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude (Pierre Kwizera 61st), Haruna Chanongo, Said Ndemla (Shaban Kisiga 38th), Elias  Maguri, Amri Kiemba (Ramadhani Singano 82nd)  and Emmanuel Okwi.

 Yanga: Deogratias Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub,  Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima (Simon Msuva 70th), Geilson Santos (Hamisi Kiiza 82nd), Mrisho Ngassa, Andrey Coutinho.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments