Ticker

6/recent/ticker-posts

SOMA KAULI ZA JOSE MOURINHO BAADA YA MAKOCHA WA ASTON VILLA KUKATAA KUMPA MKONO,NA KITENDO CHA KUSUKUMWA NA WENGER

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.18,2014 SAA 08:53  USIKU

Jose Mourinho amekataa kuomba msamaha kwa sababu ya kuwapa mkono  Paulo Lambert na Roy Keane kabla ya
mchezo kumalizika ambapo Chelsea  lilishinda 3-0 dhidi ya Aston Villa mwezi uliopita.

 Bosi wa Villa Lambert na msaidizi wake Keane walikataa kupongezana na meneja huyo wa Chelsea katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge, na Keane kulezea tebia ya Mourinho kuwa ni tabia ya "kufedhehesha", akasema: ". Mchezo bado ilikuwa unaendelea,yeye anataka kufanya hivyo, siku ya Jumapili asubuhi, angepata adhabu. "

Lambert alikubaliana alipoulizwa wiki hii kama alijisikiaje kwa kitendo cha Mourinho , na kusema alikuwa "amekosa heshima" kwa kutosubiri mpaka mwisho wa mechi ndio wapeane mikono.
Lakini akizungumza kabla ya mechi ya siku ya Jumamosi Chelsea dhidi ya Crystal Palace, Mourinho aliyeonekana kukejeli kwa majibu yake, alisema: "Awali ya yote, nataka kusema kwamba nashukuru maoni"
"Nadhani wao wawili ni wakubwa nani mifano wa watu wenye heshima na Elimu nzuri sana  na kwa sababu mimi ni mtu mnyenyekevu ambaye najaribu kujifunza kila siku na kwa kila mzoefu, nashukuru maoni."
Alipoulizwa kama angeweza kufanya hivyo tena, Mourinho alijibu "ndiyo", kabla ya kurudia "hapana" alipoulizwa kama anajua watu wanamchukuliaje kwa matendo yake.
Yeye alikataa kutoa maoni alipoulizwa juu ya mapendekezo ya hatua iliotakiwa kuchukuliwa kwa jeuri.
Mourinho pia alikataa kujibu kufuatia Arsene Wenger kuomba msamaha baada ya meneja huyo wa Arsenal kumsukuma Mreno huyo katika mchezo ambao Chelsea walishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal Oktoba 5.
"Sina majibu," Mourinho aliongeza.
"Nilijibu baada ya mechi, ambapo niliwaambia hakuna kilichotokea, na wewe bado unayo majibu kutoka FA (Football Association), kamati ya nidhamu,miongoni mwenu, kwamba hakuna kilichotokea."
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments