IMEWEKWA DESEMBA 31.2013 SAA 12:55
Uongozi wa klabu ya Young Africans umewasilisha barua rasmi kwa ZFA
kutoshiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi kesho Januari Mosi 2014 Visiwani Zanzibar katika miji ya
Unguja na Pemba kutokana na
kuamua kulivunja benchi nzima la Ufundi.
Kufuatia kupewa taarifa (notice) kwa
kocha msaidzi Fred Felix "Minziro" kocha wa makipa Razaki Siwa na
daktari wa timu Nassoro Matuzya kwa sasa Young Africans haina kiongozi
wa benchi la ufundi hali inayopelekea timu kujitoa katika mashindano
hayo.
Wiki iliyopita
mholanzia Ernie Brandts alipewa taarifa (notice) ya siku thelathini (30)
na klabu ya Young Africans kusitisha mkataba wake na timu ilikuwa chini
ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa
ambao nao pia wamepewa taarifa za kusitisha ajira zao.
Kutokana
na timu kwa sasa kutokua na kocha mkuu, kocha msaidizi, kocha wa
makipa na dakatari wa timu imekua ni vigumu kwa kikosi cha Young
Africans kwenda kushiriki mashindano hayo kwani haina mwalimu hata mmoja
kwa sasa.
Hii
inafuatia uongozi wa klabu ya Young Africans kuamua kufanya mabadiliko
ya benchi zima la Ufundi kwa lengo la kuongeza tijaa katika utendaji na
kuhakikisha benchi linapata watu wa kuchukua nafasi zao na kuanza kazi
mara moja.
Aidha uongozi
unaendelea na mchakato wa kuwapata warithi watakaochukua nafasi hizo
haraka ili waweze kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya
Vodacom na mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Idadi
ya makocha waliotuma maombi ya kuomba kuinoa timu ya Yanga mpaka sasa ni
45 huku pia idadi hiyo ikiendelea kuongeza kadri siku zinavyokwenda na
uongozi unaamini utapata makocha wazuri, wenye uwezo mkubwa pia wa
kuifikisha Yanga katika hatua nyinge ya juu zaidi.
Chanzo:www.youngafricans.co.tz
0 Comments