Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 31.2013 SAA 11:05
Baadhi ya wanachama wa klabu ya simba wakizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)mapema hii leo |
Wanachama wa klabu ya Simba wamepinga hatua iliyotolewa na kamati ya shirikisho la mpira Tanzania,na kutomchukulia hatua
Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage kwa sababu ya kukiuka sheria.
Wanachama hao wamesema hayo wakati walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari hii leo, na kusema kuwa,wameamua kujiolozesha ili waweze kuitisha mkutano mkuu wa Dhalula kuanzia hii leo.
Pia wanachama hao wamesema,walitegemea Tff kuvisaidia vilabu kutoingia katika migogoro,lakini badala yake wanaendelea kwena kinyume na hinyo.
Ikumbukwe kuwa,Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtaka Rage kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa taratibu za klabu ya Simba baada ya kubaini mapungufu kadhaa ya kisheria kwenye uamuzi wa Kamati ya
Utendaji ya Simba uliofanywa Novemba 18, 2013 kwa kumsimamisha
Mwenyekiti wao.
Upungufu huo ni pamoja na ukiukwaji wa Ibara ya 33 ya
Katiba ya Simba juu uitishaji wa mkutano, ajenda ya kumsimamisha
Mwenyekiti kuwasilishwa kwenye kikao kwa utaratibu wa mengineyo.
Changamoto nyingi zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti huyo zingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Simba.
Pia Mwenyekiti ametakiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kuzingatia Katiba ya klabu hiyo.
Katika
mkutano huo wa kujaza nafasi, ndiyo utakaojadili mgogoro kati ya
Mwenyekiti na Kamati yake ya Utendaji. Nafasi hiyo kwa sasa inakaimiwa
na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Joseph Itang’are baada ya
Geofrey Nyange aliyekuwa akiishikilia kujiuzulu.
0 Comments