IMEWEKWA DISEMBA 20,2013 SAA 04:30 USIKU
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza, Jack Wilshere ameadhibiwa na chama cha soka nchini humo kutocheza mechi mbili za ligi kutokana na kupatikana hatia ya kutoa ishara ya matusi kwenye mchezo wa timu yake Manchester City.
Tukio hilo kilitokea wakati viongozi hao wa Ligi ya Premia walilazwa 6-3 na City uwanjani Etihad Jumamosi.
Kitendo hicho hakikuonekana na marefa waliosimamia mechi lakini
kilinaswa kwenye video. Licha ya kukubali shtaka hilo, Wilshere ambaye
ni mchezaji wa kimataifa wa Uingereza alikuwa amelalamika kwamba adhabu
hiyo ni kali mno.
Kidole kimekuponza kaka |
Tume ya FA hata hivyo ilikataa tetesi zake na sasa Wilshere atakosa
mechi ya Arsenal nyumbani dhidi ya Chelsea Jumatatu na safari ya West
Ham United walio nambare nne kutoka mwisho ligini mnamo Desemba 26.
Mechi zote mbili ni debi za London.
0 Comments