Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva hii leo amezungumza na waandishi wa Habari,ambapo amelitolea ufafanuzi suala la
mshambuliaji Elias Maguli ambalo limekua likichua nafasi kubwa katika baadhi ya vyombo vya habari kabla na baada ya siku ya Simba (Simba Day) kwa kudaiwa mchezaji huyo ameachwa kwenye usajili wa msimu wa 2015-16.

![]() |
| Kabla ya mkutano na waandishi wa habari kuanza |
“Elias Maguli Jina lake halikuwepo kwa vigezo ambavyo mwalimu anavijua na sisi kama wanasimba na stake holder wa mpira siku zote mmekuwa mkipiga kelele viongozi hasa wa vilabu vya Simba na Yanga mmekuwa mkiingilia majukumu ya walimu sisi tukaona tuheshimu hilo pamoja na kwamba Elias Maguli tulimsajili kwa matumaini makubwa”Evans Aveva
“Lakini mwalimu alipokuja akaona uwezo wa Elias Maguli ni mdogo kwa hiyo katika ile mechi ya Villa Elias Maguli hasishiriki, kinachofuata baada ya hapo ni maongezi pamoja na viongozi wa Simba kujua hatma yake"
Evance Aveva pia ameweka wazi juu ya hatma ya golikipa Ivo Mapunda.
Evance Aveva pia ameweka wazi juu ya hatma ya golikipa Ivo Mapunda.
"Ivo Mapunda ataendelea kuwa mchezaji wa Simba Sports club katika kipindi kinachokuja”
“Mazungumzo yalifikia hitimisho na wakakubaliana Ivo atakuja kusaini mkataba na klabu yetu ya Simba mpaka hivi ninavyo zungumza ni kwamba ni bahati usajili umesogezwa mbele, kwa hiyo bado tuna muda lakini mpaka hapa ninavyozungumza Ivo bado hajaonekana kuja kusaini mkataba Simba hivyo jukumu hili limerudishwa tena katika kamati husika na Ivo yupo bado Dar tutatoa majibu”alisema Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva
MSIKILIZE RAIS WA SIMBA EVANS AVEVA

0 Comments