Livepool leo wamesafiri kuwafuata Leicester City katika mchezo wa ligi kuu England na meneja Brendan Rodgers
amethibitisha kuwa Steven Gerrard amepewa ofa ya mkataba mpya na klabu hiyo ya Liverpool,kama kujaribu kumaliza wasiwasi juu ya mustakabali wa mchezaji huyo.
Mkataba wa sasa wa nahodha huyo wa zamani wa England unamalizika muda wake mwishoni mwa msimu, na Gerrard atakuwa na uwezo wa kusaini makubaliano ya awali ya mkataba na klabu nyingine mwezi Januari,lakini mchezaji huyo ameamua kumalizia muda wake katika uwanja wa Anfield.
Rodgers amesema kwama Gerrard angepewa wakati wowote anachokihitaji kama angeamua kuondoka, lakini anaamini uamuzi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 haukuwa wa motisha ya kifedha .
A smiling Brendan Rodgers arrives at Melwood on Monday ahead of Liverpool's trip to Leicester City (left) while Steven Gerrard was in relaxed mood while watching the Premier League action at home on Sunday (right)
Reds captain Gerrard is driven to the club's Melwood HQ for training on Monday morning
"Kwa Steven,kila kitu amekifanya akiwa hapa ,katika miaka 16 ,ni mtu ambaye anastahili heshima mkubwa na itolewe wakati huo nafikiria, kwa sababu ni hatua kubwa,"
"Kuna mambo mengi pengine ambayo Steven atakuwa amefikiria katika uamuzi kama huu, lakini nina uhakika haitakuwa fedha. Nimezungumza naye mara kwa mara na kwa kirefu na kwamba haikuwa kesi."
"Jambo moja liko wazi, Mimi nina upendo wa kufanya kazi na Steven Gerrard, yeye ni mchezaji bora ambaye anacheza katika Ligi Kuu.Ninafurahia kila dakika moja ninayofanya kazi pamoja naye hapa na mimi nina matumaini kwamba ataendelea".alisema Brendan Rodgers
Brendan Rodgers pia amekanusha habari za kuwepo kwa uhusiano mbaya kati yake na Gerard baada ya kuvuma kwa habari kuwa nahodha huyo alikerwa na kitendo cha kuwekwa benchi kwenye mchezo walioshinda bao 1-0 siku ya Jumamosi dhidi ya Stoke - mchezo ambao mchezaji huyo alikuwa akitimiza miaka 16 tangu acheze mechi yake ya kwanza na klabu hiyo ya Livepool .
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments