Ticker

6/recent/ticker-posts

SOMA ALICHOKISEMA KOCHA WA MAN UNITED LOUIS VAN GAAL BAADA YA MECHI ZAO KUANGUKIA KRISMASI NA MWAKA MPYA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.DEC.02,2014 SAA 08:38 USIKU
Manchester United Siku ya leo jumanne inakutana na timu ya Stoke city katika mchezo wa Ligi kuu England, mchezo
utakaopigwa katika dimba la Old Trafford,mchezo ambao kocha wa klabu hiyo Louis Van Gaal anaamini kuwa ni muhimu kwa Manchester United ili kudumisha kasi yao akijua kuwa  timu yake itakutana na mtihani mgumu katika michezo yao.


Pamoja na orodha ndefu ya Majeruhi, United wamekaa katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya ushindi mara tatu mfululizo dhidi ya Crystal Palace, Arsenal na Hull City.

Van Gaal anataka kuona timu yake inajisogeza juu na kujiimalisha ili kurudi katika Ligi ya Mabingwa lakini kocha huyo bado anakubali kuwa ushindani wa Ligi Kuu akimaanisha kila mchezo ni mtihani mgumu.
Mbali na kuelezea mchezo huo kocha Manchester United Louis van Gaal pia ameelezea masikitiko yake katika kipindi cha Krismasi juu ya ratiba ya Ligi Kuu.
van Gaal anasikitika kwamba hatapata kuwaona wapendwa wake wakati wa msimu wa sherehe, kwa sababu ya michezo ya England na ratiba nzito , lakini pia anahisi kuwa - ratiba hiyo ambayo itahusisha michezo minne katika siku tisa - kuwa ni sehemu ya mzigo na si haki kwa wachezaji.
Lakini kocha huyo wa zamani wa Ajax, Barcelona, ​​Bayern Munich na Uholanzi yuko tayari kukabiliana na ana matarajio mazuri kwa United.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 alisema: " sina furaha - lakini siwezi kufanya mabadiliko - kwa sababu sidhani kama ni vizuri kwa wachezaji kwamba wao wanacheza ndani ya siku mbili  mechi za (awali) - mechi mbili katika siku mbili ".
"mwezi  Desemba utakuwa kama hivyo. Sisi pia tuna familia. Nina mke na watoto, na wajukuu, na siwezi kuwaona katika Krismasi hii".
"Lakini nataka kufanya kazi katika Ligi Kuu, hivyo tutakabiliana, nami nitakabiliana. Lakini sidhani kama ni nzuri. Ni si nzuri kwa  wachezaji, wala kwa familia."
Krismasi Manchester United katika Ligi Kuu watakuwa wenyeji wa Newcastle na siku ya Boxing Day na siku mbili baadaye watasafiri kuwafuata Tottenham ,kisha watakutana tena na Stoke City Siku ya Mwaka Mpya.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments