Bingwa mpya wa dunia katika mashindano ya magali,Lewis Hamilton amelipa fadhira juu ya ushindi kwa mchezaji
mwenzake Nico Rosberg baada ya kuambatana sambamba kila mmoja kwa mara ya kwanza katika sherehe ya Mercedes, tukio lililofanyika nchini Ujerumani mwishoni mwa wiki.
Madereva hao walichuana katika mashindano ya mbio za magari yaendayo kwa kasi maarufu kama Formula one ya Abu Dhabi Grand Prix.
Hamilton alianza akiwa katika nafasi ya pili katika mashindano hayo, lakini baadaye akaanza kuongoza katika mbio hizo kutoka kwa mshiriki mwenziwe kutoka kampuni ya Mercedes, Nico Rosberg ili kutetea taji.
Some synchronised spinning from Hamilton and Rosberg
Rosberg in the Mercedes-Benz W154 from the 1930s
The fireworks go off for the new World Champion (Mercedes image)
Lewis Hamilton anasema walikuwa timu moja walipokuwa 13 na walikimbia pamoja na daima walikuwa wanazungumza kuhusu siku moja kuwa katika timu hii ya F1, hivyo anamuheshimu sana Nico Rosberg kwa kuwa hapa leo kwa ajili ya kupambana katika michuano ya dunia wakiwa pamoja.
Anasema si rahisi kuwa katika michuano kama walivyokuwa mwaka huu na kwa Nico, kwa 100% hakuwa na uzoefu na urahisi ,Lakini yeye alifanya kazi ya ajabu na baadaye kuonesha utaalamu wa hali ya juu na alionyesha heshima na kwa muda mrefu urafiki wao umekuwa kwa miaka mingi, mingi.
Lewis Hamilton aliyasema maneno hayo, katika tukio ambalo mashabiki 50,000 walihudhuria.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments