Ticker

6/recent/ticker-posts

ROLLINGSTONE:SABABU ZA KONGO KUKATALIWA KUANDAA MASHINDANO YA VIJANA NA KUPEWA DAR ES SALAAM

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.Jun. 19,2014 SAA 12:53 JIONI
Michuano ya vijana ya ROLLINGSTONE yanatarajiwa kuanza tarehe 15 mwezi wa saba mwaka huu katika jiji la Dar es
salaam.

Mashindano hayo ambayo yanahusisha timu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati yanajulikana kwa kuibua vipaji mbalimbali vya soka.

Akizungumza na Jamii na Michezo Willybroad Alphonce ambaye ni mratibu wa michuano hiyo kwa nchi za Afrika mashariki na kati amesema maandalizi ya michuano hiyo yamefikia asilimia 50 na lakini bado wanaendelea kutafuta wadau ili waweze kuwasaidia.

"Bila shaka Watanzania mtakuwa mashaidi wakubwa kuwa mashindando haya ya ROLLINGSTONE yamewai kuisaidia Taifa letu, kwa timu za chini ya miaka 17,20,23 na halkazalika katika timu ya Taifa Stars,historia inatukumbusha kuwa tuna wachezaji ambao wamepitia hapa,wakina Hamil Maftaa,Elasto Nyoni,Kigi Makasi bila kuwasaha wachezaji kama Shabani Kado japokuwa alikaa kwa muda mfupi,Lidondo,Kanavaro na katika nchi ya Burundi kuna wakina Ndikumana na wengine ambao wametokana na mashindano haya." alisema Willybroad Alphonce.

Katika mashindano hayo nchi zinazotegemewa kushiriki ni pamoja na wenyeji Tanzania,Tanzania Visiwani,Burundi,Rwanda,Kongo,Kenya na kwa mara ya kwanza nchi ya Somaria na Sudani ya kusini ambao wameomba kushiriki,pia watakuwepo.

Miaka yote mashindano hayo hufanyika Arusha kasoro mwaka juzi ambapo yalifanyika Burundi,nchi ya Kongo ilikuwa imeomba kuandaa mashindano hayo kwa mwaka huu lakini kwa sababu za kiusalama hilo halikuwezekana na kwa maana hiyo jiji la Dar es salaam ndilo limepata nafasi ya kuandaa mashindano hayo.

USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments