Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 03,2014 SAA 01:22 ASUBUHI
Kocha Jurgen Klopp amekiri kuwa timu yake ya Borussia
Dortmund "alifanya mambo rahisi sana" baada ya Real Madrid kuibuka na ushindi wa 3-0 katika Robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa usiku wa jana.
Gareth Bale alifunga bao la kwanza ndani ya dakika tatu na Isco aliongeza la pili kabla ya Cristiano Ronaldo kuhitimisha bao la tatu nakuifanya Real Madrid kujiwekea mazingira mazuri katika Ligi hiyo ya mabingwa .
Na pia katika mchezo huo, Ronaldo alionekana kuweka rekodi ya Ligi ya Mabingwa kwa mabao 14 katika msimu huu na kifanya Madrid kama kulipiza kisasi kutoka msimu uliopita baada yakutolewa katika hatua ya nusu fainali mikono mwa Dortmund.
Klopp ambaye alijitengenezea jina kwa timu yake katika mchezo wa pili baada ya ushindi wa 4-1 dhidi Real katika msimu uliopita, lakini kocha huyo alikataa lawama kutokuwepo kwa kushindwa katika mchezo wa jana.
"Ndio ni tofauti, lakini magoli tuliyofungwa usiku wa leo,hakuna kitu tulichofanya kuhusiana na hilo," alisema.
"Hatukumiliki vya kutosha.Goli la kwanza lilikuwa rahisi sana, tulifanya mambo rahisi sana kwao".
"Katika kipindi cha pili tulikuwa na nafasi nyingi na hatukujaribu hata moja kwao, lakini najua timu hii inaweza kufanya vizuri zaidi na tunafikiria." alisema Jurgen Klopp
0 Comments