Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 14,2014 SAA 05:42 USIKU
Baada ya kuipatia timu yake ya Liverpool bao la ushindi dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili, hakuna shaka kwamba
Philippe Coutinho amekuwa ni mtu ambaye amewavutia mashabiiki wengi wa klabu hiyo.
Philippe Coutinho amekuwa ni mtu ambaye amewavutia mashabiiki wengi wa klabu hiyo.
Inaonekana shabiki No 1, kwa vyovyote vile , ni mwanawe wa kiume ambaye hawezi kumsaidia uwanjani,lakini anaweza kumsaidia kwa kuimba wimbo wa kumsifia baba yake kama kumpa hamasa awapo uwanjani.
Mke wa Coutinho, Aine, aliweka video katika ukurasa wake wa Instagram akionyesha kipande cha video nzuri ambacho alionekana kijana wao akiimba kwa sauti ya kitoto 'Coutino-ooo' na 'sisi ni Liverpool' huku akuzunguka katika chumba.
VIDEO
Aine aliandika: ' shabiki mdogo mzuri katika dunia!'
Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 21 hakika anastahili pongezi kutoka kwa mtoto wake baada ya kufanya kazi nzuri siku ya Jumapili kwa kuisaidia Liverpool kuzidi kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu.
Livepool walifanya mashambulizi mapema na kuongoza kwa 2-0, shukrani kwa bao Raheem Sterling Dk.6 na Martin Skrtel Dk.26 kabla ya City kufanya makubwa katika kipindi cha pili kilipoanza.
Boa la David Silva Dk.57 na la kujifunga mwenyewe la Glen Johnson Dk.62 liliamsha matumaini City iliyokuwa ugenini katika uwanja wa Anfield, lakini Coutinho alirejesha furaha kwa timu yake iliyokuwa nyumbani kwa bao la ushindi katika dakika 78.
0 Comments