Ticker

6/recent/ticker-posts

HABARI ZA UHAMISHO:HII NDIO MIPANGO YA INTER MILAN KWA FERNANDO TORRES

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 14,2014 SAA 04:00 USIKU
Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Inter Milan Marco Fassone imethibitisha kuwa Fernando Torres ni mmoja wa wachezaji
ambaye wanavutiwa naye .

Torres anaendelea kutajwa juu ya kuondoka katika klabu ya Chelsea licha ya Jose Mourinho hivi karibuni kutangaza kwamba wana mapango naye wa baadaye kwa timu hiyo ya Stamford Bridge.

Mshambuliaji  huyo wa Uhispania pia aliweka wazi kwamba yeye bado ana nia ya kusalia kwa kujifunga kwa miaka miwili ya mwisho wa mkataba wake, ingawa ameendelea kujitahidi kushikilia nafasi yake mara kwa mara tangu kuanzia msimu huu kutokana na ushindani.

Rais wa Inter Erick Thohir hapo awali alikiri kwamba Torres ataweza kusaini mkataba mzuri kwa klabu hiyo ya Italia, na Fassone anasema bado wana mengi sana juu ya mipango yao.

Hata hivyo, Fassone amesisitiza kuwa Inter kwa sasa wanatafakari mengi  juu ya kuchagua na bado wao hawajaamua cha kufanya juu ya lengo lao.

Lengo la Inter kwa sasa ni juu ya kuhakikisha wao wanahitimu Europa League, baada ya kumaliza watisa na kuwakatisha tamaa katika Serie A msimu uliopita.

Akizungumza kuhusu Torres, Fassone aliiambia Radio Deejay: "Yeye (Torres) ni mmoja wa majina ambayo tuna maslahi kwetu, kama alivyokiri rais wetu Erick Thohir katika siku za karibuni"

"Kisha utagundua inatokana na wakati ambao tunatakiwa kuwa na mchezaji wa kuzingatia|".
"Sasa lengo letu ni kupata nafasi katika Europa League".
"Itakuwa tatizo kutocheza katika ligi ya Ulaya kwa misimu miwili mfululizo."
Inter kwa sasa ni wa tano katika Serie A, na katika Ligi ya Mabingwa UEFA wanamashaka ya kufikia, Kwani lazima wahakikishe  wanamiliki alama sita za juu ili kufuzu.

Post a Comment

0 Comments