Bosi wa Manchester City Manuel Pellegrini ana hofu kuwa kiungo muhimu wa timu yake Yaya Toure anaweza kukosa
michezo sita ya mwisho katika Ratiba yao ya ligi katika changamoto ya kuwania taji.
City wameanguka pointi saba nyuma ya Liverpool baada ya kufungwa 3-2 katika uwanja wa Anield, ingawa bado wana michezo miwili mkononi, na Toure alitolewa nje huku akichechemea katika dakika ya19 tu ya mchezo.
Livepool walifanya mashambulizi mapema na kuongoza kwa 2-0, shukrani kwa bao Raheem Sterling Dk.6 na Martin Skrtel Dk.26 kabla ya City kufanya makubwa katika kipindi cha pili kilipoanza.
Boa la David Silva Dk.57 na la kujifunga mwenyewe la Glen Johnson Dk.62 liliamsha matumaini City iliyokuwa ugenini katika uwanja wa Anfield, lakini Makosa ya Vincent Kompany yalimruhusiwa Philippe Coutinho kurejesha furaha kwa timu yake iliyokuwa nyumbani kwa bao la ushindi katika dakika 78.
Pellegrini, ambaye anasubiri kugundua kiasi kamili cha tatizo la Toure, alikiri reds wanastahili kuwa mabingwa kama wao wataongeza kushinda michezo yao inayokuja.
MChile huyo aliiambia Sky Sports: "Ni vigumu kwa Yaya kuwa katika mchezo ujao,Tutaona kesho, mimi sijui jinsi gani yeye amejeruhiwa pa kubwa".
"Nadhani itakuwa vigumu kwake kumaliza kucheza msimu huu".
"Tutaendelea kupambana, hakuna kumaliza leo"
"Kama Liverpool wameshinda michezo yao minne, ni kwamba watacheza na kushinda michezo 14 watakuwa katika mstari ambao wanastahili kuwa mabingwa, na Kama hawatashinda michezo yake manne., Sisi tuta kwenda kuwa mabingwa"
"Mshindi hawezi kumaliza leo."
Pellegrini anaona timu yake ilikuwa na bahati mbaya sana kuondoka Anfield mikono mitupu na anaamini watalipa kwa kubadilika zaidi kwa nafasi zao watazounda katika michezo inayo fuata.
0 Comments