Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 09,2014 SAA 12:08 JIONI
Pep Guardiola ana amini kuwa itakuwa 'makosa makubwa ' kama Bayern Munich watashindwa kufikia hatua ya nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga Manchester United.
Bayern walitoka sare ya 1-1 katika uwanja wa Old Trafford katika robo-fainali ya kwanza , watakuwa bila mfungaji wao wa wiki iliyopita Bastian Schweinsteiger,pamoja na Javi Martinez na Thiago Alcantara.
Guardiola ana jaribu kuiga mtindo wa mtangulizi wake Jupp Heynckes, ambaye alishinda Bundesliga, Kikombe cha Ujerumani na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona Guardiola anafahamu ugumu wa kushinda taji la tatu tena na ameamua kuwa kimya kimya katika uwanja wa Allianz Arena siku ya leo Jumatano usiku.
"Hapa tunapambana," alisema Guardiola. "Mimi sipo hapa kwa kujinganisha mimi na Jupp alivyofanya msimu uliopita".
"Tumeshindi Bundesliga, na kama sisi hatutaingia katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ni makosa makubwa kwetu"
0 Comments