Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 09,2014 SAA 09:42 ALASIRI
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney atacheza katika mechi dhidi ya Bayern Munich leo Jumatano kwa maana yake hata kama ana maumivu ya
majeraha ya sindano aliyoyapata kabla ya mchezo, kwa mujibu wa meneja David Moyes.
majeraha ya sindano aliyoyapata kabla ya mchezo, kwa mujibu wa meneja David Moyes.
Rooney alitiliwa mashaka kuwepo katika katika mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, katika uwanja Allianz Arena baada ya kuugua kidole cha mguu wakati wa mechi ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford wiki iliyopita.
Mchezaji huyo amekosa mchezo wa Ligi Kuu ambao walishinda dhidi ya Newcastle siku ya Jumamosi,lakini alishiriki kikamilifu katika mazoezi kabla ya kikosi cha United kuruka kuelekea Ujerumani.
Moyes, ambaye timu yake ilichomoza na sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa watetezi katika mechi ya kwanza,ana tamaa kubwa ya kumuona Rooney katika mchezo muhimu, hasa baada ya Robin van Persie tayari kuwa nje kwa sababu ya kuumia.
"Yeye dhahiri atacheza," alisema Moyes. " tutafanya yote ili tuweze kuwa naye katika uwanja.Hakuwa katika mazoezi wiki nzima, lakini tayari amekuwa na sindano kabla ya mchezo".
"hatukufanya kosa lolote kimatibabu,ni mmoja wawaliopo,Kama ameamua kucheza, basi tutaweza kuwa naye ."
Wakati huo huo, Moyes amekubali kuwa kila mchezaji wake ana haja ya kuwa na wakati bora dhidi ya Bayern na kwamba timu yake ina haja ya kufanya maboresho kutokana na utendaji wa mchezo wao wa kwanza ili kufikia nusu fainali.
"Ni mchezo gumu kwetu ili kufika mbali. Timu zote mbili zina wachezaji wa viwango ya juu," alisema.
"Tunaweza na tutacheza vizuri zaidi kuliko katika mechi ya kwanza na sisi tutakuwa na wacheza bora ili kuendelea".

0 Comments