Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 08,2014 SAA 11:46 JIONI
Kocha wa Paris
St Germain Laurent Blanc anataka timu yake kutumia mfumo wa
kushambulia dhidi ya Chelsea katika mchezo
wao wa Ligi ya Mabingwa hatua robo
fainali ya pili katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya leo Jumanne licha ya kuwa na
fahari ya faida mabao mawili.
PSG,
ambao walishinda michezo 11 mfululizo katika mashindano yote, wanajivunia kuongoza kwa
3-1 katika mechi ya kwanza iliyopigwa katika uwanja wa Parc des Princes wiki
iliyopita.
Baada
ya kupoteza mchezo wao mmoja tu kati ya 17 ya michezo ya Ligi ya Mabingwa , Blanc ana ujasiri timu yake itafika nusu fainali kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1995, lakini anatarajia kuwepo kwa hali ya kuzorota
kutoka kwa timu ya Jose Mourinho.
"Tunaamini baadhi ya mambo na mimi siku zote naamini kuwa tutakuwa na mchezo
wa upinzani ambao utakuwa bora kwa kushinda kikombe," alisema Blanc.
"hatujaja hapa kuteseka na basi la Chelsea tutalazimisha mchezo wetu na
kuutawala wote. Jukumu la timu iliyo juu ni kuutawala mchezo hata ukiwa mbali na
nyumbani".
"Falsafa yetu ni moja ya kushambulia,ni kama kuweka mpira na
kusababisha matatizo kama msimamo wetu. Itakuwa ajabu kujaribu
kufaulu kwa kuiacha falsafa hii katika hatua moja ama nyingine."
Mshambuliaji wa Swedish Zlatan Ibrahimovic, ambaye alifunga mabao 10 ya
Ligi ya Mabingwa msimu huu, atakosa mchezo huu baada ya kuumia mguu
katika mechi ya kwanza.
0 Comments