Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 09,2014 SAA 03:38 USIKU
Assem Allam |
Klabu ya Ligi
kuu ya Uingereza Hull City imepata utata juu ya jitihada zake za kubadili jina lao
kuwa Hull Tigers baada ya
kukataliwa na chama cha soka cha Uingereza FA , uongozi wa chama hiko umesema hii leo Jumatano katika taarifa
yake .
"Baraza
la FA, ambalo limeundwa na wawakilishi kutoka katika mpira wa miguu,
kikamilifu limepata mapendekezo kutoka kwa Hull
City na kufikia uamuzi wake," FA walisema katika tovuti yake.
Uongozi huo wa FA Umesema uamuzi ulichuokuliwa, umetokana na asilimia 63.5 kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo.
Mzaliwa wa Misri na mfanyabiashara Assem Allam aliinunua Hull Desemba 2010 na
alitangaza mipango ya kubadili jina la klabu mwishoni mwa mwaka jana katika jitihada za kuinua hadhi ya klabu hiyo nje ya nchi.
Allam anaamini kwamba nembo ya 'Tigers' “itauza zaidi ulimwenguni”.
Mashabiki sugu wa Hull waliapa kupinga hatua zozote za kubadilisha jina la klabu hiyo na wameunga kundi kwa jina "City Till We Die" (City Hadi Kufa Kwetu au City piga ua).
Taarifa kwenye tovuti rasmi ya Hull siku ya Jumatano ilisema klabu haijatoa maoni yoyote juu ya uamuzi wa FA.
0 Comments