Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 09,2014 SAA 03:38 USIKU
Meneja wa Manchester United David Moyes anasisitiza ana
malengo imara ya kuweza kuirudisha klabu yake katika Ligi ya Mabingwa.
United imetolewa nje ya michuano hiyo ya Ulaya siku ya Jumatano usiku kwa kufungwa mabao 3-1 na Bayern Munich katika uwanja wa Allianz Arena, ambapo imeyaaga mashindano hayo ya mabingwa wa Ulaya kwa jumla ya maba 4-2.
Kwa Matokeo hayo inamaanisha kwamba kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995, United hawana uwezekano mkubwa kwa sasa kurudi tena katika msimamo wa juu wa ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.
Baada ya kushindwa mjini Munich, Moyes aliiambia Sky Sports: "Hatujawa na Ligi ya Mabingwa ya mpira wa miguu, hivyo ndiyo tunavyoona, lakini naamini kwamba si mbali mbali, na natumaini itakuwa ni mwaka mmoja baadaye.
"Tunaenda kujijenga na lengo letu ni kupata timu ambayo inaweza kurejea katika shindano hili, na shindano kubwa ambalo kweli tunalifurahia na hakuna aibu kwa kutolewa nje na Bayern Munich".
Moyes pia aliulizwa kama anaamini kazi yake inaweza kuwa katika mashaka makubwa, baada ya kushindwa kwake kupata kucheza katika Ligi ya Mabingwa.
"Hilo si swali langu kwa sababu kazi yangu ni kuhakikisha tunabaki juu na kufanya kazi," alisisitiza.
"Nimetafuta kila mtu katika klabu nzuri sana na malengo yangu ni kuifanya timu yetu kurudi katika Ligi ya Mabingwa na hilo ndilo lengo kuu."
Moyes anasisitiza kwamba uongozi wa klabu hiyo ina muuunga mkono na mipango yake ya kujenga timu na tayari kuna hamasa, na anasisitiza kutokuwa katika Ligi ya Mabingwa hakutodhoofisha kutekeleza azma yao yoyote ya malengo yao ya juu.
"Klabu hawajawahi kuwa na matatizo yoyote, hakuna kitu chochote kinachosemwa , klabu inaangalia matumizi ya fedha vizuri juu ya wachezaji wazuri ambao wanapatikana, hakuna kitu unachoweza kufanya katika Ligi ya Mabingwa ya mpira wa miguu," alisema.
"Mchezaji Yoyote tunazungumza naye kimya kimya na nadhani wao wana furaha zaidi ya kujiunga na Manchester United.
"wale ambao wako kimya kimya,wanaweza kuwa na neno wamesikia, wote wamekuwa na nia ya kuja na ni jambo la muda mfupi, si kitu cha muda mrefu na wote wana nia sana ya kujiunga na klabu kubwa."
0 Comments