Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 09,2014 SAA 09:38 ALFAJIRI
Arjen Robben amekiri kwamba Bayern Munich walizinduka wakati Patrice Evra alivyoipatia Manchester United bao la
kuongoza dhidi yao katika Ligi ya Mabingwa ya hatua ya robo fainali katika mchezo wa pili.
Baada ya beki huyo wa Ufaransa kuiweka mbele timu yake iliyokuwa ugenini katika dimba la mjini Munich la Allianz Arena, na kuwafanya MaBavarian hao kuchomoa bao hilo kwa sekunde 69 tu baada ya Mario Mandzukic kutumbukiza mpira kwa kichwa.
Thomas Muller kisha akaipatia Bayern bao la kuongoza kabla ya Robben kufunga bao la tatu na kuwafanya mabingwa hao mabingwa watetezi kutinga hatua ya nusu fainali.
"walifunga bao la kwanza hivyo bila shaka ilikuwa ni vigumu, lakini mwisho 3-1, ni matokeo mazuri sana," alisema winga huyo wa zamani wa Chelsea akiiambia Sky Sports.
"Nadhani ni muhimu sana tulifunga moja kwa moja baada ya wao kufunga. Ilikuwa kuna umuhimu leo, inaonekana kama tuliamshwa kwa sababu dakika 10 za kwanza katika kipindi cha pili walikuwa wazuia njia ya sisi kucheza".
"Tulikwenda polepole, hatukuwa katika mchezo na huwezi kufanya hivyo katika Ligi ya Mabingwa -. Utaweza kuadhibiwa,kipi tunatakiwa kufanya , lakini tuliamka na kufunga mabao matatu.
"Tulitaka kushambulia na kucheza mpira wetu,wao walikuwa kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi - ni hatari sana na wachezaji wakubwa wako mbele ambao wana haraka sana"
"Tulikuwa makini sana. Katika kipindi cha kwanza sisi tulidhibitiwa kimchezo, katika kipindi cha pili iliongezeka, ni mbaya sana na tungefungwa, lakini kwa bahati nzuri tukageuka wote."
0 Comments