Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 15,2014 SAA 01:35 USIKU
Mwanasoka mkongwe wa Brazil Pele alijiunga katika sherehe ya timu ya New York Cosmos katika msimu wa
ufunguzi wa ligi na kupata nafasi ya kupiga picha na sanamu iliwekwa kwa kumbukumbu yake.
 |
Pele akiwa na sanamu yake wakati wa timu yake ya zamani New York Cosmos ilipocheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Atlanta Silverbacks
|
 |
History: Pele alitumia miaka yake miwili na timu ya zamani ya New York Cosmos katika miaka ya 1970
|
Pele, ambaye alicheza soka katikati timu ya zamani ya Cosmos katikati ya miaka 1970,aliangalia timu yake hiyo ya ligi ya soka kutoka Amerika ya Kaskazini ikipata ushindi wa 4-0 dhidi ya Atlanta Silverbacks siku ya Jumapili.
Kama mgeni maalumu wa sherehe hizo,Pele ambaye anachukuliwa kama kioo, alipewa nafasi ya kuangalia jezi mpya za timu hiyo.
 |
Nyota wa Zamani wa Newcastle na England, Alan Shearer pamoja na sanamu yake mwaka 2011
|
 |
Gary Lineker akiiba crisp kutoka kwa sanamu yake katika makumbusho huko London mwaka 1998
|
 |
Nyota wa tenisi wa Uingereza Andy Murray akisimama na sanamu yake katika uwanja wa Tennis Classic mwaka 2007
|
 |
Kevin Keegan akitabasamu huku akimchana nywele sanamu yake,ilikuwa ni mwaka 1976
|
 |
Wayne Rooney nyota wa Uingereza sanamu yake ikiwa katika mji wa Shanghai
|
 |
Mkongwe wa Ufaransa Zinedine Zidane akionesha dole kandokando ya sanamu yake iliyowekwa katika mji wa Madrid mwaka 2002
|
Meneja Bret Pidgeon, aliiambia SoccerNation kuwa 'Pele ya ni mtu muhimu kama kivutio kwao na kuongelea pia na historia yake ndani ya mchezo wa soka na kwingineko.
'Sisi tuna furaha kubwa kwamba tuna mtu ambaye ilikuwa ni sehemu muhimu na tunashukuru kwamba tunaweza kuwa na furaha na New York Cosmos katika ufunguzi wa ligi ya nyumbani.
Pele, sasa ana umri wa miaka 73, alicheza michezo 56 na alifunga mabao 31 wakati wa miaka miwili aliyoitumia katika timu ya New York Cosmos katika miaka ya 1970.
0 Comments