Ticker

6/recent/ticker-posts

MANCHESTER UNITED KUTOA OFA YA KUSTUA KWA KUMNYAKA KIUNGO WA BARCELONA ILIYOPIGWA MARUFUKU KUUZA WALA KUNUNUA WACHEZAJI

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 16,2014 SAA 08:00 USIKU
Manchester United make shock move for Barcelona midfielder Song

Manchester United wanatarajia kutoa ofa ya kustua kwa
kiungo wa Barcelona Alex Song kwa mujibu wa Mtandao wa Goal.


Mashetani hao wekundu wameonyesha kuwa wako tayari kutumia kiasi cha £12.5 million kwa ajili ya mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal. 

Liverpool, AC Milan na Atletico Madrid pia wamejisogeza karibu katika mbio za kumtaka Song, ambaye anatarajiwa kuondoka Camp Nou msimu huu , lakini mtandao huo umesema unaelewa kuwa United wako katika nafasi ndogo kwa ajili ya kumchukuwa nyota huyo wa kimataifa wa Cameroon ikiwa ni hatua ya meneja David Moyes juu ya mipango wa kuimarisha nafasi ya kiungo wa kati. 

Moyes, ambaye pia ana malengo na mchezaji wa Bayern Munich  Toni Kroos,ambaye meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola  amesisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi, kwani bado anamuhitaji kusalia katika klabu hiyo.

Na mchezaji mwingine ambaye Moyes anamalengo naye ni kutoka Sporting Lisbon, William Carvalho, lakini amevutiwa zaidi na uwezo wa kiungo Song kama kuweka vizuri eneo la beki wa kati. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameonekana katika katika mechi 28 kati ya 53 za Barcelona katika mashindano yote ya msimu huu lakini pia ameanza katika mechi 12 tu na mabingwa hao mara 43 wa ligi na mechi za Ligi ya Mabingwa.

Lakini ikumbukwe kuwa Fifa imepiga marufuku Barcelona  kusajili na kuuza wachezaji kwa vipindi viwili vya uhamisho lakini dili hili halita izuia klabu kuuza wachezaji. 

Makamu wa Rais Manel Arroyo alisema wiki iliyopita kuwa Barca wamekata rufaa dhidi ya uamuzi katika jitihada za kuokoa uamuzi huo wa kupiga marufuku maswala ya usajili na kwamba "timu yetu ya kisheria inafanyia kazi ili tutaweza kuwa na uwezo wa kuwa na wachezaji wapya msimu huu  wa majira ya joto".

Song alijiunga na Arsenal kutoka klabu ya chini Ufaransa Bastia akiwa 
mwenye umri wa miaka 18 na miaka saba akatumika katika Uwanja wa Emirates, ambapo alijiimarisha sehemu muhimu ya kiungo kwa kocha Arsene Wenger kabla ya kufuata nyayo za Cesc Fabregas na kuhamia Barcelona.



Post a Comment

0 Comments