Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 16,2014 SAA 09:53 ALASIRI
Bosi wa Manchester City Manuel Pellegrini anasisitiza hana
majuto kuhusu kumuanzisha Vincent Kompany katika mechi dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili.
Kumekuwa na wasiwasi juu ya Kiongozi huyo na maamuzi yake katika mbio za ubingwa wa ligi kuu,na nahodha wa City Kompany alikuwa ana uuguza tatizo la goti alilopata katika mazoezi.
Hata hivyo, mchezaji huyo aliingizwa katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Anfield na timu hiyo kupokea kuchapo cha mabao 3-2.
kidole cha lawama kinaweza kumwelekea Kompany kwa ajili ya mabao yote matatu dhidi ya Liverpool,kutokana na kiwango chake alichokionesha katika mchezo.
Ingawa Pellegrini, anadai yeye alifanya maamuzi sahihi ya kumuita kwa manufaa na nahodha huyo alikuwa fit vya kutosha kuiongoza City katika vita vya Merseyside.
Akasema: "Alianza mchezo kwa sababu yeye ni nahodha".
"Yeye aliweka ushahidi wote kabla ya mchezo, alisema ilikuwa sawa na daktari alisema hivyo,mimi sijutii hili".
"Lakini mimi sipendi kuchambua uchezaji wa mtu binafsi katika vyombo vya habari".
"Nazungumza na wachezaji wakati sisi tukishinda au kupoteza, ni jukumu la timu nzima."
Kompany amepata nafasi ya kurudi katika kikosi cha City katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Sunderland siku ya leo Jumatano.
Pellegrini aliongeza juu yeye kukabiliwa na changamoto ya wachezaji majeruhi msimu huu: "Sisi tunacheza msimu mzima na majeruhi wengi".
"Sasa tuna Yaya - tulikuwa na Kompany, Aguero, (Samir) Nasri".
"Tulikuwa ni timu pekee ambayo iliendelea katika mashindano manne kwa sababu tulikuwa na kikosi muhimu na wachezaji wengi wao wanacheza vizuri".
"Yeye (Toure) ni mchezaji muhimu, mmoja wa watu muhimu zaidi ambao tunao katika timu yetu".
"Lakini katika kikosi chetu, lazima tupate mbadala katika wakati huu. Nina hakika tutakwenda kufanya hivyo na hakuna tatizo." alisema Manuel Pellegrini
0 Comments