Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS:FIFA WASITISHA ADHABU YA BARCELONA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 23,2014 SAA 10:56 JIONI
Barcelona transfer ban suspended
Fifa imetangaza kuwa wamesitisha athabu waliyoipa timu ya  Barcelona ya kuwapiga marufuku kusajili wala kuuza
wachezaji, baada ya timu hiyo kusajili wachezaji wenye umri mdogo,kufuatazo rufaa ya Barca dhidi ya adhabu waliyopewa. 

Balcelona walipigwa marufuku kusaini wachezaji kwa vipindi viwili vya uhanisho baada ya kukiuka maadili ya kanuni na sheria zinazohusiana na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji chini ya umri wa miaka 18, lakini uamuzi huo umesimamishwa mpaka uamuzi wa mwisho dhidi ya rufaa yao utakapochukuliwa. 

Kwenye taarifa yake iliyochapishwa hii leo kwenye mtandao wa fifa.com na kwa klabu ya FC Barcelona, imetoa kibali kwa timu hiyo kufanya usajili wakati wa dirisha dogo wakati ikisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake iliyoikata kwenye shirikisho hilo.

"Klabu ya Barcelona imetuma rufaa ya kukata mbele ya Kamati ya Rufaa ya Fifa dhidi ya uamuzi wa kamati ya Fifa ya nidhamu kwamba klabu ilisababisha ukiukaji wa uhamisho wa kimataifa na usajili wa wachezaji chini ya umri wa miaka 18. Pamoja na kukata rufaa,ombi la klabu kwa rufaa yake limefunguliwa kwa kusimamisha athabu, "inasomeka taarifa rasmi. 


FC Barcelona imesema inaheshimu sana maazimio yaliyotolewa na bodi husika  kwa kutenda haki. "


Sheria hii inasema kuwa klabu inaweza kusajili mchezaji wa chini ya miaka 18 iwapo wazazi wa mchezaji huyo wamehamia kwenye nchi husika, pili iwapo wazazi wa mechazaji huyo wanatokea kwenye nchi za Ulaya na ukanda wa kiuchumi na tatu iwapo mchezaji wa umri wa miaka 16 na 18 anaishi umbali wa kilometa 100 toka makao makuu ya klabu hiyo.

Uamuzi huu wa fifa umekuja wakati muafaka, wakati huu klabu hii ikihusishwa na kutaka kufanya usajili wa kipa wa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani, Marc-Andre ter Stegen na pia kutaka kumsajili kiungo Mcroatia Alen Halilovic.



Nahodha wa kitambo kwenye timu hiyo, Carles Puyol pamoja na mlinda mlango wao Victor Valdes wote kwa pamoja wametangaza kuachana na timu hiyo itakapofika mwishoni mwa msimu huu.


Post a Comment

0 Comments