Ticker

6/recent/ticker-posts

MACHESTER UNITED WAMETHIBITISHA HILI KUHUSU PAUL SCHOLES

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 23,2014 SAA 10:11 JIONI
Manchester United wamethibitisha kuwa Paul Scholes yuko katika uwanja wa mazoezi wa klabu Carrington  kwa ajili ya
kumsaidia bosi wa muda wa klabu hiyo Ryan Giggs.

Mashetani hao wekundu walitoa taarifa  ifuatayo kupitia Twitter ikisema: "Ni jambo kubwa kumuona Paul Scholes katikauwanja wa mazoezi hapa leo  akisaidiana na Ryan Giggs, Nicky Butt na Phil Neville."

Scholes, mwenye miaka 39, ni mkongwe katika uwanja wa Old Trafford baada ya kuwa katika safu ya wachezaji wa United ambao wamecheza mechi zaidi ya 700 katika timu ya kwanza.

Scholes amejiunga na kocha anayemaliza muda wake Phil Neville na Nicky Butt katika kumsaidia mchezaji mwenzao wa zamani Giggs katika juhudi zake za mwisho wa msimu kuisaidia timu hiyo ya Old Trafford.


kufuatia kufungishiwa virago kwa David Moyes siku ya Jumanne,Moyes atalipwa fidia ya £5million baada ya kufukuzwa kazi na Manchester United – ikiwa ni kipengele cha makubaliano ya mkataba wake na klabu hiyo.

Moyes ambaye ni Kocha wa zamani wa Everton amekaa miezi 10 tu katika mkataba wake wa miaka 6 na, hatua hiyo imekuja baada ya kuwa na mfululizo mbaya wa matokeo.

Katika mkataba wa Moyes na United kulikuwa na kipengele kinachoeleza ikiwa Manchester United ingeshindwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa msimu huu,na United wakaamua kusitisha mkataba wake basi fidia isingezidi mshahara wake wa miezi 12 ambao ni £5million.

Post a Comment

0 Comments