Ticker

6/recent/ticker-posts

ALICHOKISEMA ROBERTO MARTINEZ KUHUSU LUKAKU,BAADA YA TETESI KUWA MOURINHO ANATAKA KUMUUZA MCHEZAJI HUYO

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 12,2014 SAA 09:54 ALASIRI
Roberto Martinez anaamini itakuwa ni 'kitu kikubwa' kama Romelu Lukaku atakaa katika klabu ya Everton na ana amini
mshambuliaji huyo anafurahia mpira .


Lukaku amefunga mabao 14 akiwa na Everton msimu huu tangu kuwasili kwa mkopo kutoka Chelsea kabla ya uhamisho wa mwisho wa majira ya joto, lakini mustakabari wake wa baadaye bado haijajulikana.


Mchezaji huyo ameanza mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu kwa Chelsea tangu uhamisho wake 2011 kutoka Anderlecht na kumekuwa na uvumi kwamba Jose Mourinho atamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 katika majira ya joto.

Martinez ana imani ya kumuona nyota huyo wa kimataifa kutoka  Ubelgiji anakaa katika uwanja wa Goodison Park na ameelezea maoni yake kwamba Everton wanaweza kutoa ofa yenye 'furaha' kwa Lukaku .


" Hatuchezi kamari juu yake tunafanya mambo vizuri kwa sababu tunajua nini anaweza kuleta na tuko kamili katika suala hilo," alisema meneja Everton.



"Kama tunaweza kutanua mkataba wake,itakuwa ni vizuri. Kama siyo, tutakuwa na kumbukumbu kubwa".


"Nadhani kuna kitu tunatoa ambacho hawezi kupata mahali pengine,anafurahia mpira wake hapa".alisema Roberto Martinez

Post a Comment

0 Comments