Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea,Mechi
ya raundi ya 25 ya Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ashanti
United inachezwa Jumapili (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi nyingine zitakuwa jumamosi kati ya Tanzania Prisons na
Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal
Union itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Keshokutwa (Aprili 13 mwaka huu) kutakuwa na mechi
nyingine nne za kukamilisha raundi hiyo. Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa
Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
0 Comments