Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 30,2014 SAA 08:O0 USIKU
Kocha Tim Sherwood amejihami mapema kwa kutubu baada makosa kutoka kwa timu yake ya Tottenham kwa kufungwa
4-0 na Liverpool.
Spurs ilikuwa nyuma baada ya dakika ya pili tu,baada ya Younes Kaboul kudumbukiza mpira wavuni mwake mwenyewe, na kisha dakika ya 25 Luis Suarez kupachika bao la pili la kuongoza kabla ya kwenda mapumiziko.
Na Sherwood anakubali kwamba timu yake haiwezi kumudu kupata njia nafuu ya mabao dhidi ya Liverpool.
"Mchezo ilikuwa umemalizika baada ya makosa mawili," aliiambia Sky Sports.
"Unaweza kufanya mipango yote bora lakini wakati tulipofanya makosa mapema, tulidhani tena tutakaa katika mchezo bora , lakini tulimaliza katika muda wa dakika mbili na sisi tukajaribu kurudu nyuma lakini wao walikuwa na nafasi mzuri na wao walikuwa na imani kubwa kutokana na goli la kwanza, kila mtu daima alikuwa hivyo,goli la kwanza ni muhimu lakini sisi tumefungwa na timu bora leo".
"Mtu yeyote anaweza kufanya makosa, ni aibu tu sisi tumepata adhabu kama tulivyofanya."
Pamoja na Tottenham kushindwa dhidi ya Liverpool, ina maana rekodi yao dhidi ya timu nne za juu msimu huu ni sare moja na kufungwa mara saba, na mabao mawili tu walifunga - na Sherwood anakubali hali ni si nzuri vya kutosha.
0 Comments