Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:MKONGWE RYAN GIGGS AONYESHA HISIA ZA KUJIAMINI MBELE YA BAYERN MUNICH

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 30,2014 SAA 11:50 JIONI
Ryan Giggs anasema  wala hafikirii timu yake ya Manchester United kuwa dhaifu siku ya Jumanne katika Robo fainali ya
kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich katika uwanja wa Old Trafford.

Giggs ilikuwa ni sehemu ya kukosi cha United kulichowapiga Bayern 2-1 katika  fainali ya Ligi Mabingwa mwaka 1999 katika uwanja wa Camp Nou wa klabu ya Barcelona, na kufanikiwa kutwaa kombe hilo kutokana na  magoli ya dakika za majeruhi kutoka kwa Teddy Sheringham na Ole Gunnar Solskjaer, na sasa anatarajiwa kuwepo siku ya Jumanne pia katika mpambano huo mkubwa.

Alipoulizwa ukilinganisha United ya sasa na ya mwaka 1999, alisema:. "Ni wazi kwamba wachezaji ni tofauti lakini mila na klabu bado ni sawa, klabu mbili kubwa, mbili zenye historia kubwa na timu za soka mbili ambazo hucheza mpira wa miguu kwa njia sahihi".

"Wakati Bayern inapocheza na Man United daima ni mpambano mkubwa iwe ni katika fainali ya Ligi Mabingwa au ikiwa katika robo fainali".

"Ni wazi kwamba Bayern ni timu yenye uwezo. Wao ni mabingwa watetezi na ni wazi kuwa wana timu kali sana na pengine ni mabingwa katika macho ya watu wengi. Lakini sisi ni Manchester United,tutakuwa katika uwanja wa Old Trafford na tumecheza mara nyingi hasa katika michuano ya Ulaya".

"Kama wachezaji hatuoni kama tutakuwa na hofu, sisi wenyewe tunaona kama Man Utd inacheza nyumbani katika Ligi ya Mabingwa na hatuwezi kusubiri".

"Huu ni michezo ambao unatakawa kushiriki  kama mchezaji na sisi tutakwenda kwao na kujaribu kushinda mchezo,itakuwa ngumu lakini ni kawaida ni katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na tunajiamini. "

Post a Comment

0 Comments