IMEWEKWA JANUARI 9.2014 SAA 10:43 ALFAJIRI
Kiungo wa Real Madridi Xabi Alonso amebainisha kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili ya kubaki kuichezea klabu hiyo ya nchini
Spain.
Nyota huyo wa kimataifa wa
Hispania aliyekuwa anatiliwa shaka katika miezi
ya hivi karibuni kuhusu mkataba wake uliopita ulikuwa unamalizika mwishoni
mwa msimu.
Hata
hivyo, mchezaji uyo wa zamani wa Liverpoo hatimaye ameweka nia ya mustakabali wake kwa
Santiago Bernabeu kwa kuendelea kukaa katika
klabu hiyo hadi majira ya joto ya mwaka 2016.
Muhispania huyo alitoa ujumbe katika akaunti yake rasmi ya Twitter kwa kutangaza habari,
akiongeza kuwa alikuwa "na furaha sana" na kuongezewa kukaa kwake.
Alonso, ambaye alijiunga na klabu ya hiyo mwaka 2009, aliweka wazi mapema mwezi huu kwamba yeye alikuwa na hamu ya kushinda vikombe zaidi na Madrid - ikiwa ni pamoja na kombe la 10 la klabu bingwa ulaya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amecheza katika michezo 12 kwa msimu huu, lakini kwa sasa ametengwa kwa sababu ya tatizo la ndani ya sikio lake na amelazimika kukaa nje katika ushindi wa siku ya jumatatu dhidi ya Celta Vigo.

0 Comments