Yaya Toure amekuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kutangazwa usiku wa kuamkia
leo.
Kiungo huyo wa Manchester City amewapiku wachezaji wawili akiwemo Mnigeria John Obi Mikel(nafasi ya pili) na mwenzake wa Ivory
Coast Didier Drogba(nafasi ya tatu) na kuwa mshindi wa mara tatu wa tuzo hiyo,na kuwa sawa na
Abedi Pele pamoja na Samuel Eto'o.
Mghana Abedi Pele alishinda mara tatu katika kati ya miaka 1991 mpaka 1993 wakati Mcameroon Eto'o alichukua tuzo mwaka 2003 na 2005.
Eto'o, ambaye anacheza katika klabu ya Chelsea, pia alishinda mwaka 2010.
Kocha bora wa mwaka kwa Afrika ni Stephen Okechukwu Keshi.
Na mchezaji bora wa mwaka anayechezea Afika ni Mohamed Mohamed Mohamed Aboutrika
0 Comments