Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 17,2014 SAA 10:06 JIONI
Real Madrid jana iliondoka na ushindi baada ya bao la Galeth Bale kuiwezesha timu yake hiyo kunyakuwa kombe
la Copa Del Rey katika mchezo wa fainali wa kombe hilo uliomalizika kwa timu hiyo kuichapo Barcelona kwa mabao 2 kwa 1.
Angel Di Maria ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia Madrid bao la kuongoza katika dakika ya 11 ya mchezo huo.
Baada ya kipindi cha pili Barca walifufua matumaini baada ya kusawazisha bao hilo kupitia kwa Marc Bartra dakika ya 68,lakini juhudi zao zilikatishwa na mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili Galeth Bale kwa bao lake dakika ya 85,na kuifanya timu hiyo kuondoka na kombe hilo pasipo kuwa na Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa nje kwa sababu ya majeraha.
0 Comments