Tim Sherwood anaamini Tottenham ingeweza kuwa na changamoto
katika mbio za kupata taji la ligi kuu msimu huu kama bado Gareth Bale angekuwa katika timu yao.
katika mbio za kupata taji la ligi kuu msimu huu kama bado Gareth Bale angekuwa katika timu yao.
Bale, 24, alikuwa mahiri kwa Spurs msimu uliopita, na alifunga mabao 26 katika
mashindano yote, kabla ya kuuzwa katika majira ya joto kwenda Real Madrid kwa uhamisho ambao ni rekodi ya dunia kwa kiasi cha £ 85m.
Mchezaji huyo amekuwa vizuri kwa timu ya Hispania katika msimu huu, kwa kufunga mabao 20 katika
mechi 38, ikiwa ni pamoja na goli alilotumia nguvu binafsi siku ya Jumatano usiku katika fainali ya Copa del
Rey dhidi ya Barcelona.
Tottenham,
ambao pia walimuuzwa kiungo Luka Modric kwa Real Agosti 2012 kwa ada iliyoaminika kuwa ni karibu na £ 33m, timu hiyo inajitahidi ili kudumisha changamoto za kufuzu katika
Ligi ya Mabingwa msimu ujao, sasa ni wa sita katika msimamo, pointi saba
nyuma ya Arsenal walioko katika nafasi ya nne.
Alipoulizwa
kuhusu bao la Bale aliloshinda katika ushindi wa Real 2-1 dhidi ya
Barca, Sherwood alijibu: "Hiyo ni biashara kwa kawaida kwa Gareth Bale".
"Tuliona aliyoyafanya mwaka jana: mabao 21 na kusaidia mara tisa, alifunga mabao ya ushindi katika mechi nane".
"Tunaweza
kufanya kwa sasa, kwa njia yeyote. Kama tukichukuwa pointi zote na zitakazotuweka kuwa juu pengine tutakuwa katika changamoto za kugombea taji".
"Wachezaji wawili bora uwanjani jana usiku (katika fainali ya Copa del Rey ) walikuwa ni Gareth Bale na Luka Modric na nasema hivyo kwa kila
kitu."
Spurs watakutana na Fulham siku ya Jumamosi kwa lengo la kuziba pengo kati yao na timu iliyokuwa katika nafasi ya tano Everton.
Sherwood
alikiri kwamba ushiriki wa timu yake katika Europa Ligi msimu huu ulikuwa umeiweka timu yake katika mzigo mkubwa , lakini alikuwa na nia ya kuwaona vijana wake wakimaliza na nguvu kama ingewezekana.
0 Comments