IMEWEKWA JANUARI 10.2014 SAA 09:14 USIKU
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amepigwa faini ya £ 8,000 na kuonya juu ya tabia ya kutoa maoni yasiofaa dhidi ya muamuzi wa mechi yao na Manchester City, mwezi uliopita ambayo
walipoteza, baada ya yeye kukiri kwa shirikisho la FA kufuatia utovu huo wa
nidhamu.Katika taarifa ya FA inasema hivi: "Rodgers ameshtakiwa kwa uvunjaji wa kanuni E3 ya FA baada ya kutoa maoni baada ya mechi kufuatia mchezo wa Liverpool na Manchester City Desemba 26, 2013 kilitokana mwenendo mbaya kwa kosa linaloitwa uadilifu wa mwamizi katika mechi,/na alisema kuwa mwamuzi alikuwa na motisha ya upendeleo katika mechi ; /na kuleta mchezo kwa jina baya./ na walishindwa kuchukua hatua kwa maslahi ya mchezo "
Rodgers alishangazwa kwa nini refa wa kutoka eneo la Greater Manchester
aliteuliwa kuamua mechi hiyo waliopoteza 2-1 na kutaja kazi yake kama ya
‘kutisha’ akielekezea gadhabu yake kwa Lee Mason na wenzake.
“Nilishangaa tunacheza na Manchester na referee ni wa kutoka Greater
Manchester. Nina uhakika hatuwezi pata wa kutoka Wirral (karibu na Liverpool) wakati tutawaalika City nyumbani.”alisema Rodgers.
Rodgers alikanusha baadaye kuwa maoni yake yalinuia kuzua maswali ya vile waamuzi wanateuliwa katika ligi hiyo.
0 Comments