Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.13.2016 SAA 12:18 JIONI
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) akizungumza na makocha ambao wamefuzu
kozi ya ukocha ngazi ya Intermidiate, iliyofanyika Temeke, Dar es
Salaam. Hafla hii imefanyika leo.
|
Rais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amewazawadia makocha wapya
27 waliofuzu
kozi ya ukocha kwamba kila mmoja mmoja atampa koni 20 na vizibao
22 kwa ajili ya mazoezi.
Rais Malinzi
alitoa ahadi hiyo wakati wa hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya
‘Intermidiate’ kwa makocha waliohitimu. Rais Malinzi alialikwa na waratibu kuwa
mgeni rasmi ambaye awali, alishangazwa kwa namna ilivyoratibiwa kwa kufuata
miongozi ya TFF na CAF.
Katika hotuba yake, Rais
Malinzi aliwataka waamuzi hao kuzingatia weledi wakiwa ni mabalozi wa kupinga
matumizi ya dawa za kulevya lakini zaidi wajiepushe kwa njia yoyote ile kupanga matokeo.
Rais Malinzi alifurahishwa
na idadi kubwa ya makocha waliohitimu kwani kabla walikuwa ni wachezaji wa timu
kubwa na kongwe mbalimbali, “Hilo sasa linanisukuma kuwapa kila mmoja wenu koni
20 na bips (vizibao) 22,” alisema Rais Malinzi.
Alitumia nafasi hiyo
kuwataka Watanzania kuwaombea dunia Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla
Tenga ambaye anawania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wa FIFA kwa nchi
zinazozungumza Kiingereza ambako anapambana na Kwesi wa Ghana.
Pia katika mkutano huo Mkuu
wa CAF utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia ukihusisha nchi 53 kati ya 54
wanachama wa CAF, pia watapiga kura kuichagua Zanzibar kuwa mwanachama kamili
wa shirikisho hilo.
Kozi hiyo iliendeshwa na
Wilfred Kidao - Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF), akisaidiwa na Manyika Peter aliyefundisha programu au mtaala kwa makocha
wa makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao kuhusu tiba za
wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.
Wahitimu wa kozi hiyo
walikuwa Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke pekee kati ya wanafunzi 27 walisoma
kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14 cha mwanzo wa mwaka. Doris ni mwanahabari za
michezo aliyehudhuria kozi hiyo. Anaandikia gazeti la MwanaSPOTI linalotolewa
na Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi (MCL).
Wengine ni nyota wa zamani
wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliopata kuchezea klabu
kongwe na kubwa nchini. Wanafunzi hao ni Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent
Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.
Wengine ni Omar Kapilima,
Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf,
Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud Selemani, Haji Mustapha, Mhasham Khatib, Issa
Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda,
Ally Mbonde na Evod Mchemba.
MALINZI AMLILIA SIR GEORGE KAHAMA
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, ametuma rambirambi kwa familia ya marehemu
Sir George Kahama aliyefariki dunia Jumapili akiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Rais Malinzi amesema taifa limepoteza mmoja
wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania maendeleo ya mpira wa miguu
baada ya kupigania Uhuru ambao Watanzania leo wanajivunia amani.
Pamoja na familia ya marehemu, ndugu, jamaa
na marafiki, Rais Malinzi Dkt Magufuli amewapa pole wanachama wote wa Chama Cha
Mapinduzi, akisema ni kielelezo cha kiongozi aliyetukuka.
“Kabla ya Uhuru Mzee wetu, Mzee Kahama
alikuwa kiongozi shupavu na mzalendo, alama ambayo ametuachia sisi Watanzania
leo hii tunajivunia amani,” alisema Rais Malinzi.
Rais Malinzi ambaye katika vikao vyake vya
jana hapa Dar es Salaam, alikuwa akitoa nafasi ya kumkumbuka Sir George, akisema
msiba huo pia ni wa TFF kwa kuwa mmoja wa watoto wake, Joseph ni Mjumbe wa
Mfuko wa Bodi ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu wa TFF.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali
pema peponi, Amina.
0 Comments