Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.13.2016 SAA 12:29 JIONI
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga (kushoto), akitangaza kikosi cha nyota 26 wa timu hiyo mbele ya wanahabari leo. Kulia ni Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas. |
Kocha Mkuu wa
timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga leo Jumatatu
Machi 13, 2017
ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaounda kikosi hicho.
Taifa Stars,
inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi
28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Katika mkutano
wake na wanahabari uliofanyika leo Makao Makuu ya TFF, yalioko Uwanja wa
Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni
walinda milango, Aishi Manula (Azam
FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa
pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto
wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
Mayanga
aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar),
Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam
FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
Kadhalika wako
viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil
Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC).
Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe,
Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC)
wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC
Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu na AFC
Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu(Kagera Sugar) na Abdul-Rahman
Mussa (Ruvu Shooting).
Pia Mayanga
aliwataja wasaidizi wake kuwa Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata wakati Meneja
wa timu upande wa ufundi atakuwa mwenyewe Mayanga na upande wa mipango mingine
atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa Richard
Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert
Kigadya.
Timu hiyo
itaingia kambini Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam na
mara baada ya michezo hiyo kambi itaahirishwa Machi 29, mwaka huu.
0 Comments