Ticker

6/recent/ticker-posts

HARRY REDKNAPP AKANUSHA LOIC REMY KUFELI VIPIMO VYA AFYA NA LIVERPOOL,HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.28,2014 SAA 09:49 USIKU
Meneja wa QPR Harry Redknapp amekanusha madai kwa uhamisho wa Loic Remy kwenda Liverpool ilishindikana kwa
sababu ya kufeli vipimo vya Afya.

Mshambuliaji huyo wa kimaaifa wa Ufaransa, 27, ilikuwa anatakiwa kwa ada ya £ 8.5 million   na klabu hiyo yaAnfield - huku kukiwa na taarifa za kukataliwa kwa sababu ya kufeli vipimo vya Afya- lakini Redknapp alikiri kutatanishwa na taarifa hizo na alipendekeza kungekuwa na mazungumzo ya chinichini na Liverpool kumaliza mpango huo.
Harry Redknapp
Redknapp aliwaambia waandishi wa habari: "Atarudi hapa mimi peke yangu ndiyo najua nini nilichokiona na kusikia na sihitaji kujua kama kweli alifeli vipimo vya Afya."

"Alifanyiwa vipimo na masharti magumu akiwa hapa,moja akiwa Newcastle anapocheza kwa mkopo, na moja na timu yake ya Taifa Ufaransa kabla ya Kombe la Dunia,alikuwa hana tatizo na mwili wake -. Hakuweza kukutana na daktari sahihi"

"Sioni kama kunaweza kuwa suala lolote kwa mwili wake. Hasara yao ni faida yetu. Mimi nimepata mshambuliaji mzuri."alisema Harry Redknapp.

ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments