Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.13.2016 SAA 12:29 JIONI
Timu ya taifa ya mpira wa miguu
ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys imeanza
mazoezi rasmi leo Machi 12, 2017 kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
Serengeti Boys itakuwa kambini
Dar es Salaam hadi Machi 26, mwaka huu ambako itakwenda Bukoba mkoani Kagera
kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kujiandaa na michuano Afrika ambayo
sasa itaanza Mei 14, 2017 badala ya Mei 21, mwaka huu.
Michezo ya
kirafiki ya kimataifa itakuwa ni dhidi ya timu za vijana za Rwanda (Machi 28,
2017), Burundi (Machi 30, mwaka huu) na Uganda Aprili 2, mwaka huu). Michezo
yote itafanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Timu hiyo
itarejea tena Dar es Salaam Aprili 3, mwaka huu ambako siku inayofuata itaagwa
kwa kupewa bendera na mmoja wa viongozi wa nchi kabla ya kusafiri Aprili 5,
mwaka huu kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.
Timu hiyo
itaunganisha kwenda Cameroon Mei mosi, mwaka huu ambako Mei 3, 2017 itacheza
mechi ya kwanza na Cameroon kabla ya kurudiana Mei 6, mwaka huu na siku
inayofuata itakwenda Gabon.
Serengeti Boys ni timu ya vijana
ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon
kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa
watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lalengo ya kurejea na Kombe la Afrika kwa
vijana.
La ikitokea imekosa nafasi hiyo
angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina
tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka
huu.
Kikosi cha Serengeti Boys
kinaundwa na Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin
Kayego.
Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson
Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick
Vitalis Nkosi.
Viungo: Kelvin Nashon
Naftali, Ally Ng’anzi, Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Najim Mussa,
Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.
Washambuliaji:
Muhsin Malima Makame, Yohana Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na
Abdul Suleiman.
Benchi la Ufundi:
Bakari Shime (Kocha
Mkuu)
Oscar Mirambo (Kocha
Msaidizi)
Muharami Mohamed (Kocha
wa makipa)
Kim Poulsen (Mshauri wa
Ufundi)
Edward Evans (Mtunza
Vifaa)
Shecky Mngazija
(Daktari wa timu)
Gomez Dardenne (Mtaalamu wa saikolojia)
0 Comments