Fifa imekataa Rufaa ya mshambuliaji wa Uruguay na Liverpool Luis Suarez ya kupinga adhabu ya kupigwa
marufuku kwa miezi minne kujishughulisha na soka kutokana na kumuuma mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.
Suarez pia amepigwa marufuku mechi tisa za kimataifa baada ya tukio hilo lililotokea katika kombe la dunia nchini Brazil.
FA ya Uruguay alielezea adhabu hiyo ya Fifa kama "ni uamuzi mkubwa mno" ambao "haukuwa na ushahidi wa kutosha".
Suarez sasa anaweza kukata rufaa katika mahakama ya usuluhisho ya michezo .
Serikali hiyo ya Kimataifa ya soka pia imempiga faini ya 100,000 faranga za Uswiss (£65,000) Suarez,ambaye aliomba radhi kwa tabia hiyo isiyopendeza katika Soka.
0 Comments