Samir Nasri amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na Manchester City ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya
Barclays.
Kiungo huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 mustakabali wake sasa na klabu hiyo utakuwa hadi mwaka 2019 ambapo yeye,amefurahia kuzaliwa upya chini ya uongozi wa Manuel Pellegrini na msimu uliopita, alifunga mabao 11.
'Najisikia furaha sana kusaini mkataba huu na kujua mustakabali wangu wa baadaye na City,' Nasri alisema katika tovuti ya klabu hiyo.
0 Comments