Uongozi wa Azam FC, una matarajio makubwa ya kukamilisha dili la kumuuza kiungo mshambuliaji farid Mussa Malick
ambaye juzi alirejea nchini akitokea Hispania alipokua akifanyiwa majaribio kwenye klabu ya Diportivo Tenarife inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
ambaye juzi alirejea nchini akitokea Hispania alipokua akifanyiwa majaribio kwenye klabu ya Diportivo Tenarife inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Afisa mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad kawemba amesema kwa sasa kinachofanyika ni kupangwa kwa mazungumzo kati yao na viongozi wa klabu ya Diportivo Tenarife ili kuangalia namna ya mkataba wa Farid utakavyokua endapo atafanikisha azma ya kucheza soka barani Ulaya.
Hata hivyo Kawemba ameonyesha kusikitishwa na taarifa zilizokua zikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, wakati mchezaji huyo akiwa Hispania kwa ajili ya majaribio.
Kawemba pia amezungumza kwa undani nini kinachofuata baada ya Farid Mussa kurejea nchini mwishoni mwa juma lililopita, akitokeaa nchini Hispania ambapo tayari ilisemekena mchezaji huyo amefaulu majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
MSIKILIZE SAAD KAWEMBA

0 Comments