Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:TAARIFA ZA SIMBA KUSAKA KOCHA MPYA,JACKSON MAYANJA AVUNJA UKIMYA...msikilize hapa...

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.23,2016 SAA 02:00 USIKU
Kulia:Jackson Mayanja akisalimiana na Dylan Kerr (PICHA NA www.thecitizen.co.tz)
Wakati fununu zikiendelea kushika kasi kuhusu kusakwa kwa kocha mpya wa klabu ya Simba ambaye ataaminiwa na uongozi
wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao, kocha aliye madarakani kwa sasa Jackson Mayanja, amesema haoni sababu ya kuzipa nafasi kubwa taarifa hizo kichwani mwake.
Mayanja ambaye alikabidhiwa kikosi cha Simba mwanzoni mwa mwaka huu, baada ya kuondoka kwa Dylan Kerr, amesema anatambua bado ni kocha wa Msimbazi na kwa sasa anakabiliwa na jukumu la kukamilisha ripoti ya msimu wa 2015-16 ambao ulifungwa rasmi hapo jana.
Amesema jambo kubwa ambalo ataendelea kujivunia kwa msimu huu ni mafanikio ya kukibadilisha kikosi cha Simba na kufikia hatua ya kushinda michezo 17.
Hata hivyo Mayanja alishindwa kujizuia na kuweka bayana furaha yake kwa vijana ambao amewasaidia na kufikia lengo la kuonekana katika medani ya soka la Tanzania tangu akiwa na klabu ya Coastal Union na kisha kujiunga na Simba.
MSIKILIZE JACKSON MAYANJA
KKikosi cha Simba kimemaliza msimu vibaya, baada ya kukubali kufungwa mabao mawili kwa moja katika mchezo uliochezwa jana kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam dhidi ya maafande wa JKT Ruvu.

Simba wamemnaliza wakiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu wa soka Tanzania bara kwa kufikisha point 62, wakitanguliwa na Azam FC wenye point 67 na Young Africans wapo kileleni kwa kufikisha point 73.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .



Post a Comment

0 Comments