Uongozi wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC umetangaza rasmi kuanzadaa kuandaa michuano ya vijana ya
Afrika Mashariki ‘Azam Youth Cup 2016’itakayoanza Juni 1-5 Mwaka huu.
Mwenyekiti wa Azam FC Said Mohamed, amesema dhumuni kubwa la kuanzishwa kwa michuanop hiyo ya vijana, ni kutaka kuendeleza sera ya soka la vijana ambalo limekua likipigiwa kelele kila kukicha na shirikisho la soka nchini TFF.
Said Mohamed, amesema tayari wameshafanikisha mpangio wa kuzipata timu shiriki katika michuano hiyo ambayo imepangwa kuunguruma kwenye uwanja wa Azam Complex, uliopo nje kidogo ya jijini la Dar es salaam maeneo ya Chamazi.
“Moja ya madhumuni ya kuanzisha Azam FC ni kukuza soka la vijana, kwa hiyo kwa kusisitiza hilo leo tunatangaza kuandaa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki, kutakuwa na timu kutoka Kenya, Uganda na Tanzania, wenzetu wote duniani waliopata maendeleo walianza chini huku kwa vijana na wakapanda juu, hawakuanza juu ndio wakashuka chini.
“Hivyo kuwa na timu kubwa pekee hakutoshi lazima uwe na timu za vijana ili hao vijana ndio wawe chemchem ya kuweza kupatikana maendeleo ya mpira,” alisema.
Kwa upande wa afisa mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad kawemba amesema dhumuni kubwa la kuandaliwa kwa michuano hiyo sio kuona soka likichezwa na vijana pekee yake, bali wamedhamiria kujifunza baadhi ya mambo kutoka katika timu nyingine ambazo zitatokea nje ya nchi.
Naye Kocha Mkuu kituo cha kulea na kuendeleza vijana cha Azam FC (Azam Fc Academy), Tom Legg amesema michuano hiyo itakua ni nyenzo kubwa kwake kwa ajili ya kuendeleza mikakati ya klabu ya Azam ambayo inatazama mbali katika soka.
Amesema anaamini michuano hiyo itakua na manufaa makubwa kwa kila timu shiriki kutoka katika ukanda wa Afrika mashariki, na pia itasaidia kwa klabu nyingine ambazo zitakua zikifuatilia kwa ukaribu.
Timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo ya vijana ni Azam FC Academy (Dar es Salaam), Future Stars Academy (Arusha), Football for Good Academy (Uganda) pamoja na Ligi Ndogo Academy (Kenya).

0 Comments