Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:MO AJITOKEZA NA KUTOA SABABU ZA KUTAKA KUWEKEZA SIMBA SC

  Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 29,2016 SAA 11:30 JIONI
Mfanyabiashara kijana na mwenye mafanikio makubwa nchini, Mohammed Dewji amesema angependa kuwekeza kwenye klabu ya
soka aipendeyo ya Simba ili kubadili mfumo wa kutegemea wadhamini na kuingia katika mfumo wa kujiendesha.

Dewji maarufu kama “MO”, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kwamba bajeti ya klabu ya Young Africans na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji katika michuano ya soka hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.
Mo kutokana na hali hiyo amesema yuko tayari kutoa Shilingi bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.


Hata hivyo Mohamed Dewji ametoa angalizo kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba ambao wamekua na mawazo tofautu na mpango alionao dhidi ya Simba, kwa kuaambia hana nia mbaya kama anavyofikiriwa zaidi uya kuangalia namna ya kuondoa Simba hapa ilipo na kuipeleka katika hadi tofauti.
Wakati huo huo Mohamed Dewji “Mo” akatumia nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari kulitolea ufafanuzi suala ambalo linazungumzwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba kuhusu kushindwa kwake kuziendesha klabu za Afrika Lyon pamoja na Singida United,kwa  kusema sababu iliyompelekea kuzishindwa klabu hizo ni kutokuwa na mashabiki.
 

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

 

Post a Comment

0 Comments