Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.10.2016 SAA 01:29 USIKU
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
imeagiza sekretarieti ya TFF kutoa wito mwingine kwa wanafamilia
watatu wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) walioshitakiwa mbele ya kamati
hiyo.
Walioshitakiwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ni Mwenyekiti wa RUREFA,
Blassy Kiondo; Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, James Makwinya na Kaimu Katibu
Mkuu wa RUREFA, Ayoub Nyaulingo.
Madai dhidi ya wanafamilia hao wa mpira wa miguu ni kudharau
maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF ya kuwataka wasimamishe mchakato wa uchaguzi
wa Mkoa mpaka rufaa zilizowasilishwa TFF zitakaposikilizwa.
TFF ilipeleka mwito wa kuwataka watuhumiwa hao kwenda kujibu
madai hayo mbele ya Kamati ya Nidhamu, Machi 8, mwaka huu lakini watuhumiwa
hawakutokea kwa sababu mbalimbali.
Lakini Kamati kwa kuzingatia kanuni ya Nidhamu iliona ni vyema
watuhumiwa wakapata nafasi tena ya kuja kujitetea mbele ya kamati hiyo na kama
ikitokea wameshindwa kufika, basi watume wawakilishi wao au utetezi kwa njia ya
maandishi katika kikao kingine kitakachofanyika Machi 15, mwaka huu saa 12.00
jioni kama barua inavyojieleza.
0 Comments