Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.10.2016 SAA 01:07 USIKU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), linazitakia la kheri timu za Tanzania, Young Africans na Azam FC ambazo
zina mechi za
kimataifa zitakazofanyika kesho na keshokutwa.
Young Africans ya Tanzania na Zanaco
ya Zambia utakaochezwa Jumapili kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika pia
Azam FC ya Tanzania na Mbabane Swalows ya Swaziland kuwania Kombe la Shirikisho
barani Afrika.
Maandalizi yote miwil ya kimataifa,
yamekamilika ambako Young Africans dhidi ya Zanaco, zitacheza kesho Jumamosi
Machi 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00
jioni. Waamuzi kutoka Djibouti ndio watakaochezesha mechi hiyo.
Waamuzi hao ni Djamal Aden Abdi
ambaye atapuliza kipenga wakati wasaidizi wake ni Hassan Yacin na Farhan Salime
ilihali mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Djamal. Kamisha katika mchezo huo Na. 61
atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.
Kiingilio katika mchezo huo kwa
mujibu wa Mratibu wa Mechi za Kimataifa wa Young Africans, Mike Mike ni Sh
20,000 kwa VIP ‘A’, Sh 10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya Rangi ya
chungwa, kijani na bluu) ni Sh 3,000.
Azam wao watacheza Jumapili Machi 12, mwaka huu na Mbabane
Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Waamuzi watakochezesha mchezo huo
wanatoka Benin ambao ni Mwamuzi wa kati, Addissa Abdul Ligali na wasaidizi ni
Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina huku Mwamuzi wa akiba
akiwa Moumouni Kiagou na kamisha wa mchezo atakuwa Mohamed Omar Yusud wa Kenya.
Kiingilio katika mchezo huo kwa
mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ni Sh 10,000 kwa VIP, Jukwa
Kuu itakuwa ni Sh 5,000 na Mzunguko itakuwa ni Sh 3,000.
Wakati huohuo, tiketi za waamuzi wa
Tanzania walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuchezesha
mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto Louis 2000 ya
Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo, wamepata tiketi zao za kusafiri.
Katika mchezo huo ambao utafanyika ama Machi 17, 18 au 19
Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati wasaidizi wake watakuwa ni
Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Hery
Sasii. Kamisha katika mchezo huo Na. 78 atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka
Afrika Kusini.
0 Comments