Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.10.2016 SAA 12:00 JIONI
Wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) likirejesha nyuma kwa wiki moja, timu ya taifa ya mpira wa miguu
ya vijana wenye umri
wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys inatarajiwa
kuanza kambi mpya Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Serengeti Boys itakuwa kambini Dar
es Salaam hadi Machi 26, mwaka huu ambako itakwenda Bukoba mkoani Kagera kwa
ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kujiandaa na michuano Afrika ambayo
sasa itaanza Mei 14, 2017 badala ya Mei 21, mwaka huu.
Michezo ya kirafiki ya kimataifa itakuwa
ni dhidi ya timu za vijana za Rwanda (Machi 28, 2017), Burundi (Machi 30, mwaka
huu) na Uganda Aprili 2, mwaka huu). Michezo yote itafanyika Uwanja wa Kaitaba,
Bukoba mkoani Kagera.
Sababu za kuwa na mechi hizo Bukoba ni
kupunguza gharama kwa TFF kwani ni rahisi kusafirisha timu hizo kutoka nchi
jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.
Timu hiyo itarejea tena Dar es Salaam
Aprili 3, mwaka huu ambako siku inayofuata itaagwa kwa kupewa bendera na mmoja
wa viongozi wa nchi kabla ya kusafiri Aprili 5, mwaka huu kwenda Morocco kwa
ajili ya kambi.
Timu hiyo itaunganisha kwenda Cameroon
Mei mosi, mwaka huu ambako Mei 3, 2017 itacheza mechi ya kwanza na Cameroon
kabla ya kurudiana Mei 6, mwaka huu na siku inayofuata itakwenda Gabon.
Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo
imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia
Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi
Mali, Niger na Angola. Ina lalengo ya kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
La ikitokea imekosa nafasi hiyo
angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina
tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka
huu.
0 Comments